Martin Kadinda adai RC Makonda Hakukosea Kumtaja Wema Sepetu
Meneja wa zamani wa Wema Sepetu, Martin Kadinda amedai Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Paul Makonda hakukosea kumtaja Wema Sepetu kwenye list yake ya watuhumiwa wa biashara haramu ya madawa ya kulevya kutokana na aina ya marafiki ambao amekuwa nao.
Akiongea na Bongo5 wiki hii, Martin amedai yeye alitumia nguvu nyingi kumshauri muigizaji huyo kuachana na marafiki wasioeleweka.
“Nadhani nilishakaa na Wema nikamwambia jina lako ni kubwa sana, unatakiwa kuwa na nguvu usiwe maarufu tu. Kwahiyo hichi ambacho kimetokea siwezi kuliongelea kwamba ni jambo baya au zuri lakini nadhani hii ni alarm ya kuamka,”
Aliongeza, “Sidhani kama mkuu wa mkoa alikurupuka tu akamtaja Wema, wametajwa watu wengi, labda ni kutokana na marafiki aliyokuwa nao au magroup au labda kuna mtu alienda kule akamwambia mkuu wa mkoa Wema anashiriki jambo hili, kwahiyo sidhani kama mkuu alikurupuka akamtaja Wema hapana. Lazima kuna chanzo ndiyo maana nasema ngoja tuangalie kwa sababu bado kesi iko mahakamani tutajua tu,”
Martin amedai Wema anatakiwa kubadilika na kujitenga na watu ambao wanaweza kumwingiza katika matatizo kama aliyotokea.