-->

Mastaa Hawa Wataoana 2017?

WAKATI wakielekea kumaliza mwaka 2016 bila ndoa, wasanii hawa wamekuwa mvuto mkubwa kwa mashabiki wao huku wengi wao wakiwatarajia ndoa kwa mwaka ujao wa 2017.

Diamond na Zari

Mapenzi ya msanii Nassibu Abdul (Diamond) na mwanadada kutoka Uganda, Zarinah Hassan (The Boss lady), yameboreshwa zaidi baada ya kuishi zaidi ya miaka mitatu na kupata watoto wawili wa kike na wa kiume.

Licha ya kutokufanikiwa kufunga ndoa na aliyekuwa mpenzi wake Miss Tanzania mwaka 2006, Wema Sepetu, mashabiki wake wengi wanamtarajia mwaka 2017 atimize ndoto hiyo kwa mpenzi wake wa sasa Zari ambaye ni mwanamuziki na mfanyabiashara.

Ali Kiba na Jokate

Jokate na Ali Kiba

Licha ya wapenzi Ali Kiba na Jokate Mwegelo ‘Kidoti’ kupitia katika uhusiano wa kimapenzi na mastaa mbalimbali wa ndani na nje ya nchi, wawili hao wameonekana kuwavutia mashabiki wao hasa wanapokuwa pamoja mijumuiko mbalimbali ikiwamo kwenye sherehe, mpira na mingine mingi.

Ali Kiba anayejishughulisha na sanaa ya uimbaji kwa sasa anatamba na wimbo wake wa ‘Aje’, huku Kidoti akijishughulisha na masuala ya urembo ikiwamo biashara ya nywele, ndala, nguo na muziki wapo katika mastaa wanaodhaniwa kufunga ndoa mwakani sasa ni je, nao watafunga ndoa mwaka 2017 kama wanavyodhaniwa na wengi?

Nahreel na Aika

Hawa ni wapenzi wanamuziki wa muda mrefu tangu walipokutana nchini India walipokuwa masomoni, uhusiano wao umeongeza uimara katika kundi lao la Navy Kenzo. Nahreel jina lake kamili ni Emmanuel Mkono na Aika Marealle.

Zaidi ya miaka nane katika uhusiano wa kimapenzi ndio unaowavutia mashabiki wao wakitamani wapenzi hawa waoane 2017.

Jux na Vanessa

Wapenzi hawa walianza muda mrefu tangu Jux alipoachana na Jack ambaye sasa anatumikia kifungo huko China. Wawili hawa wanatamba na wimbo wao wa Juu. Ukaribu wao na picha za kimapenzi kila wanapokuwa mapumzikoni huku kila mmoja akiwa wazi kumuelezea mwenzake inaonekana kuwa chachu ya wawili hao kuwa pamoja katika ndoa, Je, wawili hawa watafunha ndoa mwakani huku kila mmoja akionekana kuzidi kutotaka kubadili dini kumfuata mwenzake?

Lady Jaydee na Spicy

Baada ya mwanamuziki Judith Wambura ‘Lady Jaydee’ kuachana na aliyekuwa mume wake mtangazaji, Guardina G. Habashi maarufu Captain, sasa ameangukia katika penzi la prodyuza na mwanamuziki raia wa Nigeria, Spicy.

Licha ya mapenzi, wawili hao kwa sasa wanatamba na wimbo wa ‘Together Remix’, ukaribu wao na namna wanavyozungumzwa kwenye mitandao ya kijamii pamoja na watu wao wa karibu, je, nao watafunga ndoa mwaka 2017?

Lulu na Majizo

Mbwembwe na vituko vingi vya mwigizaji, Elizabeth Michael ‘Lulu’, vinaonekana kufikia mwisho baada ya kudondokea kwenye mapenzi na mwasisi wa kituo cha redio Efm mwenye umaarufu wa jina la Dj Majizo. Majizo anaelezwa kummiliki vyema mrembo huyo kiasi kwamba tabia na matukio ya utata yaliyokuwa yakimwandama mrembo huyo hayaonekani kwa sasa. Je, nao watafunga ndoa mwaka 2017 kama wanavyodhaniwa na wengi?

Moses Iyobo na Aunt Ezekiel

Mapenzi ya mcheza dansi wa Nasibu Abdul, ‘Diamond Platinumz’, Moses Iyobo na mwigizaji Aunt Ezekiel yanazidi kusonga mbele huku mtoto wao akiongeza upendo kati ya wawili hao kiasi kwamba muda wote wanatamani kuwa karibu naye.

Anty Ezekiel kabla ya kudondokea kwa Mose aliolewa na mfanyabiashara wa magari anayefahamika kwa jina la Papaa Sunday Demonte, ambaye kwa sasa anatumikia kifungo huko Dubai. Je, nao watafunga ndoa mwaka 2017 kama wanavyodhaniwa ama la?

Shilole na Adam Suleiman

Mwigizaji, mwanamuziki na mama ntilie, Zuwena Mohamed (Shilole) baada ya kumwagana na Nuh Mziwanda kwa sasa amedondokea kwa mfanyabiashara wa nguo, Adam Suleiman ambaye kiumri anaonekana kuwa mkubwa zaidi ya Shilole ambaye awali alikuwa akisemwa vibaya kwa kuwa na uhusiano na wanaume wenye umri mdogo.

Umri na namna ambavyo mfanyabiashara huyo kutokuwa maarufu kunaelezwa kuwa ni sababu kubwa ya wawili hao kufika mbali katika uhusiano wao kiasi kwamba huenda wakaoana mwaka 2017.

Harmonize na Wolper

Msanii wa Bongo Fleva kutoka Kundi la Wasafi, Rajabu Ibrahim (Harmonize) na Jackline Wolper, licha ya maneno ya kukatisha tamaa wapenzi hawa wamekuwa wakiendelea na maisha yao bila kujali maneno ya watu, je, nao watafunga ndoa mwaka 2017 kama wanavyodhaniwa?

Giggy Money na Moj

Wapenzi hawa Giggy Money na Moj walianza uhusiano wa kimapenzi muda mrefu wakati Moja akimtumia Giggy kumpata rafiki yake na ikawa hivyo, lakini baada ya kukutana pamoja katika kipindi cha Usiku redio ya Choice FM wakaanza kupendana zaidi hadi sasa ni wapenzi.

Giggy kwa sasa amepunguza upigaji wa picha za hovyo kutokana na kazi anayoifanya na aina ya mwanaume aliyenaye, huku kazi yake ikimpa nafasi ya kukutana na watu wenye nyadhifa mbalimbali. Kutokana na hayo wapenzi hawa watafunga ndoa mwaka 2017?

Young Dee na Mamisa

Licha ya rapa David Genzi kurudi kwa mpenzi wake wa muda mrefu mwenye umaarufu kwa jina la Tunda na kutoka na wimbo mpya unaoeleza kutamani kwake kumuoa, lakini inaonyesha kama imeingia dosari kwa kuwa mashabiki wengi wanatamani rapa huyo amuoe mwanamke mwingine anayefahamika kwa jina la Mamisa ambaye amejipatia umaarufu mkubwa baada ya kuweka wazi kwamba amemzalia mtoto rapa huyo ambaye awali hakuonyesha kujali, lakini baada ya kuweka wazi alijitokeza na kutoa matunzo ya mtoto wake. Je, nao watafunga ndoa mwaka 2017 kama wanavyodhaniwa na wengi?

Witness na Ochu

Kutokana na ukaribu na kuelewana katika muziki wanaofanya na mambo mengine, rapa wa kike, Witness maarufu ‘Kibonge mwepesi’ na mpenzi wake wa muda mrefu  mwanamuziki, Ochu Sheggy, nao wanatamaniwa na mashabiki wao wafunge ndoa, je, nao watafunga ndoa mwaka 2017 kama wanavyodhaniwa na wengi?

Mtanzania

Comments

comments


Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364