-->

Papaa Misifa Amuwashia Moto Upya Rich Mavoko

Meneja maarufu wa wasanii wa muziki wa Bongo Fleva nchini Papaa Misifa, ameibuka na kuzidi kumuwashia moto Msanii Rich Mavoko ambaye kwa sasa anafanya kazi na lebo ya Wasafi.

Misifa akiwa ndani ya FNL alisema Mavoko hana adabu na ni miongoni mwa wasanii wasiokuwa na shukrani kwa yale aliyowafanyia kwa kuwa yeye ndiye aliyewatoa na kuwang’arisha kwenye Bongo Fleva, lakini wamemtelekeza kwa kuvunja makubaliano.

Akizungumza jinsi alivyomsaidia Rich Mavoko, amesema tangu wimbo wake wa kwanza, yeye ndiye aliyegharamia studio.

“Sitamsahau Mavoko, alinifanyia vitu vya ajabu sana, mavoko hana heshima, kuanzia Mary me, one time nilikuwa nagharamia kila kitu hata kuna pesa nilitoa kwa ajili ya video Sauz, lakini akachukua”

Alipoulizwa endapo ugomvi wake na Mavoko ulisababishwa na pesa, Papaa Misifa akaruka na kusema “Tatizo siyo pesa, hata adabu hana”

Alipoulizwa kama endapo ana mpango wa kutumia ‘ndumba’ kumuadhibu, Misifa alisema “Hakuna uchawi ila kuna laana, hakuna uganga wowote, lakini atapata laana”

Kuhusu kumsamehe, Misifa amesema yuko tayari kumsamehe endapo atamfuata kumuomba radhi “kesi bado ipo lakini akija tuzungumze nitamsamehe”.

eatv.tv

Comments

comments


Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364