Matonya Kuja na ‘Legeza Kidogo’
Msanii mkongwe wa muziki Matonya ameweka wazi ujio wa kundi lake jipya ‘Black Image’ likiwa na project mpya ‘Mr Magufuli Legeza Kidogo’.
Muimbaji huyo ambaye kwa sasa anafanya viziri na wimbo ‘Jela’ ameiambia Bongo5 kuwa project hiyo inakuja kutetea watu wa mtaani ambao wanalalamika kuhusu ugumu wa maisha.
“Kuna project inatoka wiki hii, ‘Legeza Kidogo’ au ‘Mr Magufuli Legeza Kidogo’ ni kazi ya vijana wangu ambao walikuwa wananisumbua kwa muda mrefu niwasaidie, so nikazungumza nao na kuanzisha kundi ‘Black Image’ ili niweze kuwasaidia wasanii wote, kwa hiyo mimi ni kiongozi,” alisema Matonya.
Aliongeza, “Wimbo Mr Magufuli Legeza Kidogo ni wimbo ambao wazo nimekuja baada ya kuona malalamiko ya watu mtanii, watu wanalalamika hawana pesa, hata kile kidogo walichopata akina mama ntilie kimeondoka, kwa hiyo tumezungumzia maisha ya wananchi, hapo aliposhika Magufuli alegeze kidogo, tunajua anafanya kazi kubwa na tunaikubali lakini kwenye pesa hali sio hali,”
Pia muimbaji huyo amesema baada ya kuachia project hiyo, kundi hilo litaendelea na project mbalimbali ili kuwasaidia vijana hao kufika katika hatua fulani.
Bongo5