Davina: Filamu Imebuma, Najiongeza
MSANII wa filamu za Kibongo, Halima Yahya ‘Davina’ ameweka wazi kuwa baada ya sanaa hiyo kuonekana kubuma, sasa ameamua kujiongeza kwa kufanya biashara ya kufuata bidhaa nje ya nchi.
Akipiga stori na gazeti hili, Davina alisema baada ya kumaliza kampeni za uchaguzi ameamua kujikita kwenye biashara ya kusafiri nje ya nchi kutokana na soko la filamu kwa sasa kuwa baya tofauti na miaka iliyopita.
“Nimeamua kujiingiza kwenye biashara ndogondogo ya kusafiri nje, nitachukua biashara Mombasa, Kenya na nchi zingine na kuzileta Bongo, naamini maisha yataenda tu kwa sababu nikitegemea filamu itakula kwangu,” alisema.
Chanzo:GPL