-->

Mimi ni Demu wa Bei Kali Tukutane Mlimani City – Irene Uwoya

IRENE Uwoya muigizaji wa filamu wa kike Bongo ametamba kuwa kipaji chake ni cha kipekee kwani yeye ndio msanii wa kwanza kuanza kuigiza na kutwa tuzo kama muigizaji bora wa kike mwaka 2008, tuzo zilizojulikana kwa jina la Vinara na hadi leo bado amekuwa bora katika tasnia ya filamu Bongo.

“Ubora wangu umedumu toka kuingia katika game kutokana na misimamo yangu katika kuangalia kazi za kucheza siigizii kila filamu, unajua mimi ndio muigizaji wa kike ambaye niliingia kwenye fani kwa kutwaa tuzo,”alisema Irene.

“Naamini kuwa filamu ya Bei Kali inaleta umahiri wangu katika uwezo wangu katika kuigiza niefanya mambo makubwa sana katika filamu ya Bei Kali ni viwango vya kimataifa, Rado, Hemed na Patcho Mwamba wamekubali muziki wangu,”

Msanii huyo ambaye pia ni mjasiriamali anaamini kuwa kutoshiriki sana kuigiza kila filamu kuna mfanya asipoteze umahiri wake na ubora wake katika kuigiza sinema zinazofanya vizuri lakini pia hapendi kuigiza filamu nyingi kwa mwaka amedai kwa mwaka huu ameshiriki sinema moja tu inaitwa Bei Kali hajacheza nyingine hadi itoke hiyo.

Filamu ya Bei Kali inatarajia kuruka Mlimani City Cinema tarehe 4. 0ctober 2017 katika Golden Carpet na itaruka Mubasha kituo cha Luninga mahiri cha Azam Tv kupitia channel ya Sinema Zetu maarufu kwa filamu za nyumbani, sinema ya Bei Kali imeshirikisha wasanii nyota Irene Uwoya, Simon Mwapagata (Rado), Patcho Mwamba, Daud Michael ‘Duma’ Phd na wasanii wengine.

Filamucentral

Comments

comments


Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364