-->

Nilishakufa, Namshukuru Mungu-Ray C

Msanii wa bongo fleva Ray C ambaye awali alikuwa mtumiaji wa madawa za kulevya amefunguka na kusema yeye alishakufa ila anamshukuru Mungu kwa wema wake na kumtoa katika janga hilo la dawa za kulevya.

Ray C

Ray C alisema hayo jana alipokuwa kwenye kipindi cha Friday Night Live (FNL) na kusema leo hii yeye anasimama mstari wa mbele kama muhanga wa dawa za kulevya kupinga vita dhidi ya dawa hizo kwani zimepoteza maisha ya vijana wengi na kuharibu ndoto za watu.

“Kwangu mimi ambaye nimepitia janga hili, nimeona karaha yake yaani nilishakufa ilibaki kidogo tu, namshukuru Mungu mpaka sasa mzima kwa hiyo watu wanatakiwa hili jambo walichukulie ‘serious’ kwa sababu si janga langu wala janga la Makonda, hili ni janga la taifa nzima, mitaani wototo wanateseka sana, wazazi wanaumia, yale machozi ya wazazi, vifo vya waathirika , watu wanaotaabika, familia, kaka, dada, ndugu, jamaa yale machozi yao na maumivu yao ndiyo yanaitika sasa hivi, hivyo serikali nayo ichukue hatua kwenye jambo hili” alisema Ray C

Mbali na hilo Ray C anasema muathirika wa dawa za kulevya kumpeleka jela halimsaidii chochote hivyo ameiomba serikali kufungua vituo vya ‘Rehabilitation’ kwani anasema matumizi ya methadone hayasaidii kitu kwani zile nazo ni dawa za kulevya tu.

“Mimi nachoomba Serikali ingefungua ‘Rehabilitation’ za Serikali mbali na Methadone kwani kwangu mimi methadone bado naona ni dawa za kulevya tu, lakini ningependa sana Serikali ifungue vituo vya kusaidia waathirika wa dawa za kulevya, na ikiwezekana iwe bure kama ilivyo kwenye dawa za methadone sababu ukiambia rehab basi ni zaidi ya milioni moja na kuna watu wengine hawawezi kulipia, hivyo kuna watu wanakufa huko mitaani mimi nadhani wangeweka nguvu kwenye kuwasaidia kuwapeleka rehab kuliko kuwaanika hadharani maana kufanya hivyo ni sawa na kuzidi kuwachanganya kisaikolojia” alisema Ray C .

eatv.tv

Comments

comments


Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364