-->

TID Amtembelea Makonda Nyumbani, Afunguka Haya

Msanii wa kizazi kipya nchini TID ambaye siku kadhaa zilizopita alikuwa matatizoni akihusishwa na matumizi ya madawa ya kulevya, amefunguka na kusema muziki bila madawa ya kulevya inawezekana.

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaama Mhe. Paul Makonda akiwa na msanii TID nyumbani kwake leo.

TID ambaye leo amekutana na Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam Mhe. Paul Makonda anasema kuwa amepata nafasi ya kukaa na kujadili na kiongozi huyo kuona namna gani wanaweza kuoka vipaji vya wasanii.

“Muziki bila madawa ya kulevya inawezekana..This is the turning Point kwangu mimi na kizazi cha muziki huu wa kizazi kipya, nikiwa na Mhe. Makonda leo tukijadili jinsi gani ya kuokoa Vipaji na sanaa kwa ujumla, Mungu ibariki bongo fleva, Mungu ibariki Tanzania” aliandika TID 

Kwa upande wake Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam Mhe. Paul Makonda alikuwa na haya ya kusema baada ya TID kumtembelea leo nyumbani kwake jijini Dar es Salaam.

“Mungu wetu hajalala na siku zote anampenda amtafutae, karibu tea nyumbani T I D” aliandika Paul Makonda. 

Comments

comments


Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364