Mimi Siyo Marioo – Abubakari Mzuri
Msanii wa muziki wa Bongo Fleva Abukakari Mzuri ambaye aliwahi kutamba na wimbo kama ‘Samahani’ amefunguka na kusema kuwa yeye siyo Marioo kama ambavyo watu wamekuwa wakisema kuwa analelewa na mwanamke au ameolewa na mwanamke.
Ababukari Mzuri alisema hayo alipokuwa akihojiwa kwenye kipindi cha eNewz cha EATV na kusema kuwa yeye hajaolewa wala halelewi na mwanamke bali anaishi na mwanamke huyo na kwamba yeye ndiye anayemuhudumia kwa kuwa mwanamke huyo hana kazi yoyote anayofanya.
“Unajua mimi huyo ni mwanamke niliyekuwa naye mwanzo na sasa nimerudiana naye na kuna tetesi kuwa mimi sijui Marioo mimi siyo Marioo bali naishi na huyu mwanamke hapa hata yeye atasema hapa, baada ya vurugu kutokea hapa nimemletea nini ndani mimi siyo Marioo” alisema Abubakari Mzuri
Kwa upande wa mwanamke ambaye anadaiwa kumlea Abubakari Mzuri alikana yeye kumlea msanii huyo ingawa maelezo yake yalikuwa wazi kuwa yeye ndiye mmiliki wa vitu vingi ndani ya nyumba hiyo ambayo sasa wanaishi pamoja.
“Wale watu wamenifanyia hasara sana hapa ndani, saizi nimetoa kochi nimezipeleka kufanya ‘repair’ ila muda si mrefu nitazirudisha. Kwa hiyo watu wanasema Abubakari Mzuri ni Marioo kwangu? Mimi sina kazi na baba yupo Njenje ndiyo kazi yake hiyo lazima nimpe support katika kila hali na ndiyo inayotuweka mjini tunakula, tunavaa tunapendeza kama hivi unavyotuona, tulivyo kama mapacha” alisema mpenzi wa Abubakari Mzuri.
eatv.tv