Mke wa Roma Afungukia Roma Kuchepuka
Mke wa msanii Roma ameelezea jinsi mahusiano yake ya ndoa na rapper huyo yalivyo na kudai kuwa tabia ya wanaume kuchepuka kwenye ndoa ni wote wanayo.
Baby Mama (Nancy) huyo ambaye alifunga ndoa na Roma mwaka 2015 ameiambia XXL ya Clouds Fm kuwa ni vigumu kujua kinachoendelea nyuma ya pazia kwa mwanaume ila kutokana na urafiki na upendo kuna baadhi ya mambo kwa mumewe husamehe tu.
“Kucheat ni kwa kila mwanaume, siyo Roma tu ni vitu ambavyo vipo, unaweza ukachitiwa pasipo kujua au kwa kujua, huwezi kujua nyuma ya mwanaume kuna nini, unaweza kusema mimi namjua lakini hapana huwezi ukamjua kwa asilimia zote, sijawahi kuona kwa macho ila tabia ipo kwa wanaume ndani yao,” amesema
Kuhusu kuweza kudumu katika ndoa na mtu maarufu hasa msanii, alisema, “kikubwa ni upendo halafu kingine nilielewa kazi yake mapema, nikawaza kuhandle situation yote maana kuwa na mtu maarufu kuna vitu vingi katikati, yeye ni mwanaume, kwa kawaida wanaume wanakuwa na tabia tofauti halafu kuongeza na ule maarufu inazidi kuzaa vitu vingine tofauti,” amesema na kuongeza.
“Halafu kingine kilichosaidi kudumu mimi na Ibra ni rafiki yangu kabla hatujawa wapenzi, kwa hiyo ukiweka upendo, urafiki, hata akifanya nini unaona ngoja nimsamehe tu,” amesisitiza.
Mke wa Roma ndiye aliyepita katika media mbali mbali kutambulisha wimbo mpya wa Roma ‘Zimbabwe’ kwa madai kuwa mumewe amepata safari ya ghafla kwenda nchini Zimbabwe.