-->

Mkubwa na Wanawe Wamekuja na Matobo Kutoka Madada 6

KUNDI la muziki wa kizazi kipya la Madada Sita, ambalo lenye makazi yake Temeke jijini Dar es salaam, limeachia wimbo wa Matobo ambao wanaamini utakuja kulifanya kundi hilo kuwa miongoni mwa kundi bora la wanamuziki wa kike.

madada-sita

Akizungumza kiongozi wa kundi hilo, Christina Peter (Favell), alisema wamejipanga kufanya kazi bora ambazo zitafanya wanamuziki wengi kuunda makundi ya wanawake.

Alisema lengo la kundi lao ni kutengeneza muziki wa pamoja, ambao utakuwa na radha tofauti sana na wanamuziki wengine pia kusimamisha kundi ambalo litakuwa na nguvu.

Alisema mara nyingi kumekuwa na makundi ya wanamuziki wa kiume, lakini ya kike yamekuwa machache tena yakivungika kwa muda mfupi.

Favell alisema pia wanatarajia kufanya tamasha lao la kwanza, katika utambulisho wa bendi ya taarabu ya Yah Tmk Modern, itakayofanyika Desemba 17 katika viwanja vya Dar Live.

“Watu wategemee kazi nyingi kutoka mkubwa na wanawe, kazi ambayo itatuonesha kwamba sisi kazi tunaweza,” alisema.

Wanamuziki wengine ambao wapo katika kundi hilo ni Emmy Wimbo (Malope),Ninaah Salum (Ninaah),Lilian Khazady (Lizzy), Catherlin Richard (Catrima) na Mariam Farid (Love Mams).

Comments

comments


Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364