Nay wa Mitego: Biashara ya Mimi na Mr T Touch Ilishaisha
Nay wa Mitego anaweza akawa anamiss midundo ya producer wake wa zamani, Mr T Touch lakini hana mpango wa kufanya naye tena kazi.
Tangu waache kufanya kazi pamoja, rapper huyo amekuwa kimya kiasi na huenda akawa bado hajapata producer mwingine wa kuziba pengo lake. Akizungumza na mtangazaji wa Jembe FM, JJ, Nay amesema kuwa biashara yake na T Touch ilishakwisha.
“Katika suala ambazo huwa sipendi kuzungumzia ni suala la mimi na Mr T, tulishamalizina kama itakuja kutokea basi itakuja kutokea na kila kitu mtu ataona, nadhani hii biashara ya mimi na T ilishaisha,” alisema rapper huyo.
Kuhusu ukimya wake, Nay amesema ameamua kufanya hivyo makusudi ili kuwapa nafasi watu wengine. Amesema muda si mrefu atarejea tena akiwa na nguvu mpya baada ya kubaini kipi kinamiss kwenye muziki.
Bongo5