-->

Mkubwa na Wanawe Watoa Msaada Hospitali ya Temeke

KITUO cha kuvumbua na kuendeleza vipaji vya muziki cha Mkubwa na Wanawe, kimetoa msaada wa vifaa vya tiba na usafi, dawa za meno, sabuni, maji na juisi kwa wagonjwa waliolazwa katika Hospitali ya Temeke, Dar es Salaam.

Mkubwa-ba-Wanawe

Mkubwa na wanawe

Said Fella, alisema wameamua kufanya hivyo kutokana na kuguswa na changamoto zinazoikabili hospitali hiyo.

Alisema alishauriwa na vijana wake waliopo katika kituo chake kuona ni vipi wanaweza kushiriki katika shughuli yoyote ya kijamii kwa kipindi hiki cha mfungo wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhan na wote kwa pamoja kukubaliana kutoa msaada huo.

Akipokea msaada huo, mmoja wa madaktari wa hospitali hiyo, Rashid Nyumbiage, alikishukuru kituo hicho kwa kuwakumbuka akiwataka wasanii na viongozi wake pamoja na wengineo wenye nafasi kuendelea kuwakumbuka.

“Vifaa tulivyoletewa ni Paso-Oxymeter cha kupimia kiwango cha oksijeni mwilini, HB Culvate cha kupima kiwango cha damu, mashine ya BP ambayo kazi yake ni kufahamu kama presha ya damu (BP) imeshuka na mashine ya ‘Nebulizer’ yenye kazi ya kuwapimia dawa wagonjwa wa pumu,” alisema Nyumbiage.

Mtanzania

Comments

comments


Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364