Mkwanja Wampeleka Kidoa Bongo Movie
MUUZA nyago mwenye figa matata Bongo, Asha Salum ‘Kidoa’ amesema kuwa, miongoni mwa mabadiliko aliyoyafanya katika mwaka huu wa 2017 ni kujikita kwenye ulimwengu wa filamu kuliko mambo ya kuwa video queen.
Akipiga stori na Global Publishers, Kidoa alisema kutokana na mapenzi mazito aliyonayo upande wa maigizo na kugundua kuwa filamu zinalipa kuliko u-video queen, ameamua kujikita zaidi kwenye sekta hiyo akiamini atatimiza ndoto zake kirahisi.
“Toka kitambo ukifungua moyo wangu inaanza sanaa ya maigizo kisha ndiyo mambo ya umodo, nimeona bora nielemee kwenye kuigiza kutokana na matunda niliyovuna mwaka jana kwenye dili za filamu kwani zinalipa kuliko kuuza sura kwenye video, najua mwaka huu nitatusua zaidi,” alisema.
Chanzo:GPL