-->

Mr Blue Awakubali Diamond na Zari

Mr Blue amesema Diamond na Zari ndiyo couple anayoikubali zaidi.

mr blue190

“Ukinitoa mimi na Wahyda couple ambayo naipenda, naielewa ni Zari na Diamond,” Blue alikiambia kipindi cha The Playlist cha Times FM.

“Yaani wanapendeza unajua eeh, na Mungu amewajaalia wamepata mtoto, wanashirikiana kama marafiki kwenye biashara, wanajua kucheza na akili za raia, wanaitengeneza couple yao ya kimapenzi, wanaifanya pia inakuwa kibiashara, yaani very nice,” aliongeza.

Kwa upande mwingine Blue amesema hana kabisa bifu na Diamond.

“Sina bifu na Diamond na juzi tumekutana naye Mwanza kwenye show ya Ne-Yo alivyokuja, tumeongea vizuri, tumesalimiana, safi kabisa.”

Comments

comments


Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364