-->

Mr. Blue Kuwachukulia Hatua Hii Wanaoharibu Ndoa Yake

Msanii wa bongo flava Mr. Blue ambaye hivi karibuni alipatwa na msuko suko wa kuyumba kwa ndoa yake, kutokana na kusambaa kwa tetesi za kuwasiliana na ex wake Najma Dartan, amesema yuko tayari kumchukulia hatua za kisheria aliyesababisha ugomvi huo.

NDOA YA MR blue-1

Mr Blue akiwa na mke wake

Akizungumza kwenye Planet Bongo ya East Africa Radio, Mr. Blue amesema yeye binafsi hakuwasiliana na Naj, isipokuwa habari hizo zilipoanza alidhani ni kiki inayotengenezwa na Naj na Baraka The Prince, ili kuachia wimbo wao wa pamoja.

Mr. Blue aliendelea kusema kuwa baada ya kuona hali inazidi kuwa mbaya na ndoa yake kuwa mashakani, aliamua kumfuata Baraka na kumuuliza kuhusu suala hilo, lakini Baraka alikanusha na kusema yeye hajui chochote kuhusu hilo.

“Ile habari ilikuwa ya uongo, mwanzoni mi nilihisi Baraka na mchumba wake Najma watakuwa wameitengeneza kwa ajili ya mambo yao ya kutafuta kiki, kwa sasabu ilisemekana kuna nyimbo yao wanataka kutoa Baraka na Najma, kwa hiyo wanatafuta kama kiki kutumia ubavu wangu, nikabahatika kukutana na Baraka na kumshika mkono, na kumwambia akubali mbele za watu, akasema hajui hiyo taarifa”, alisema Mr. Blue.

Mr. Blue aliendelea kusema kitendo hicho amabcho kiliyumbisha ndoa yake hawezi kukifanya kwa sababu tayari ana mke, na hawezi kurudiana na mtu ambaye alishaachana naye, na iwapo ikithibitika ni wao kina Baraka na Najma ndio wametengeneza habari hiyo ili kupata kiki, hatosita kuwachukulia hatua za kisheria.

“Hatua za kisheria lazima zichukuliwe unajua hivi vitu sio vitu vya kuharibiana, mi sa hivi nishakuwa mtu mzima, siwezi kurudia matapishi ambayo nishawahi kuyatapika, eti nikampigie Najma sijui niwe nae, kwa sababu mimi najua mke wa kumuoa najua mwanamke wa kuwa naye ndio maana nikamchagua mke wangu, na nampenda na amenizalia watoto wazuri, kwa hiyo siwezi tena kufikiria eti kumpigia Najma, siwezi kufikiria kugombana na Baraka The Prince, kwanza hatulingani, mi wakati naanza mziki ye bado yuko shule anasoma, kama ni kweli ni wao japokuwa Baraka amenithibitishia sio wao, nikijua ni wao lazima nitafute njia ya kuwashikisha adabu”, alisema Mr. Blue

 

Comments

comments


Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364