-->

Ujumbe wa Nay Wa Mitego Kuhusu Ndoa ya Shamsa Ford

Nay Wa Mitego ameonekana kumchimba mkwara mwanaume aliyemuowa aliyekuwa mpenzi wake, Shamsa Ford.

shamsa33

Nay na Shamsa walikuwa na mahusiano mwaka 2015 japo mahusiano yao hayakufanikiwa kudumu kwa muda mrefu na kila mtu kufuata njia yake huku wakidai bado ni marafiki wa kawaida.

Kitendo cha kuolewa kwa Shamsa kinaweza kikawa kimemtoa povu rapper huyo kutokana na kipande cha video alichokiweka kwenye mtandao wake wa Instagram na kuandika ujumbe unaosomeka:

TANGAZO TANGAZO TANGAZOOOO???
Naskia my #COUSIN Kaolewaaaa Sasa uyo aliyemuoa ipo siku nitampiga Tukio Kama hiiiiiiiiiii???????????
Nina hasiraaaaaaaa????

Shamsa Ford amefanikiwa kufunga ndoa Ijumaa hii na mpenzi wake mfanyabiashara wa maduka ya nguo Rashidi Said aka Chidi Mapenzi.

Bongo

Comments

comments


Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364