-->

Mr Blue: ‘Mboga Saba’ ni Habari Kubwa

Msanii wa muziki wa Bongo Fleva, Mr Blue amesema hajawahi kupata mapokezi mazuri katika muziki wake kama aliyoyapata katika video yake mpya ya wimbo ‘Mboga Saba’

mr blue

Mr Blue

Akiongea na Bongo5 Jumatatu hii, Mr Blue amesema kuna vitu vingi vimechangia kazi hiyo kuwa kubwa kwa muda mfupi.

“’Mboga Saba’ hii ni kazi ambayo imefanya vizuri zaidi kwa muda mchache kuliko ngoma zangu zote, mara nyingi nyimbo zangu zinaanza taratibu na baadaye zinafanya vizuri, lakini kwa hii ni tofauti kabisa, ni habari nyingine kabisa” alisema Blue.

Aliongeza, “Mimi nahisi imekuwa na mapokezi makubwa kwa sababu ni kolabo, ngoma zangu nyingi nilikuwa nakuja peke yangu, kwahiyo nguvu ya Alikiba pia inaonekana ndani yake,”

Video ya wimbo huyo imeangaliwa mara 85000 ndani ya siku moja na nusu kitu ambacho hakijawahi kutokea katika kazi zake zilizopita.

Mr Blue amewataka mashabiki wa muziki wake kuendelea kusupport kazi zake.

Bongo5

Comments

comments


Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364