-->

Snura Afunguka Kupigwa Chini Kwa ‘Script’ ya Video Mpya ya Chura

May 4 2016 serikali kupitia wizara ya Habari,Sanaa,Utamaduni na Michezo waliufungia wimbo wa Chura pamoja na kumfungia msanii Snura kimuziki kisha May 5 msanii huyo akawa amekamilisha vitu vyote kisha akafunguliwa kimuziki,kazi ikawa kwenye kuuachia wimbo wa Chura ambao aliambiwa aurudie,kitu unachotakiwa kufahamu kwa sasa,ni kwamba Snura aliandika script ya video lakini pia ilikataliwa.

snura45

Snura

‘’Nilipeleka script a video mpya ta Churs bodi ya filamu ilichukua muda kidogo kuipitia nilifuatilia sana ndio nikapewa majibu baada ya wao kukaa kikao na kupitia wakaniambia kuwa ile script hwajaikubali nishuti kwasababu wanasema maudhui yake yanataka kufanana na ile video ya mwanzo nilishindwa kuelewa kwasababu kwa uelewa wangu niliona nimeandika kitu tofauti kwasababu video ya mwanzo ilikuwa imechezwa kwenye maji na wanawake ndio walikuwa wanacheza lakini video hiyo ambayo niliyokuwa nimeiandika ilikuwa ni mimi mwenyewe ndio nitakuwepo kwenye hiyo video halafu sichezi natembea huku naimba halafu watu wananiona mie natembea huku naimba na wao wananifuata kwa nyuma huku wanacheza naenda napanda daladala na wao wanapanda nikishuka na wao wanashuka huku wakicheza’’ Alisema Snura.

cloudsfm

Comments

comments


Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364