-->

Msambwanda Wangu wa Kinyakyusa Nimezaliwa Nao-Witness ‘Kibonge Mwepesi’

Staa wa bongo fleva Witness aka Kibonge mwepesi  amewajia juu mashabiki wanaomsema vibaya kutokana na umbile lake, na kusema wanachukia kuona wanapendana na mpenzi wake Ochu Shegy licha ya ubonge alionao.

Witness aka Kibonge mwepesi

 

Kwenye ukurasa wake wa Instagram Witness ameandika waraka akiwaambia watu hao kuwa hajali wasemayo, kwani umbile lake hilo amezaliwa nalo na sio la kununua.

 

“Wakati mwingine watu hawanichukii mimi huchukia namna tunapendana mpenzi wangu Ochushegy, wanasema mineno kibao, roho zinawauma mpaka wanaona ni heri waanze kuni attack kwa kunitukana na wanaanza kunisakama nia yao siyo nipunguze mwili, nia yao nipunguze tako langu la kinyakyusa a.k.a #msambwanda, basi nina waahidi nitapungua kote siyo tako langu la kinyakyusa, sijalinunua dukani nimezaliwa nalo, not chinese not imported, ndo maana sijisumbui kununua wala kuongeza matako feki kama nyie”, aliandika Witness na kuweka picha yake hiyo hapo juu.

Comments

comments


Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364