-->

Nisifieni Kabla Sijafa – Said Fella

Meneja wa wasanii na kiongozi wa ‘Mkubwa na Wanawe’, ambaye pia ni diwani wa kata ya Kilungule Said Fella au Mkubwa Fella, amewataka watu kutambua mchango wake kabla hajafa badala ya kuponda jitihada zake

Said Fella au Mkubwa Fella

Akizungumza kwenye Planet Bongo ya East Africa Radio, Said Fella amesema watu wamekuwa wanaongoza kumsema vibaya badala ya kumsifia na kumpongeza, kwani kazi anayoifanya ni kubwa.

“Alafu kuna watu wanasemaga Said Fella sijui kawafukuza Yamoto, leo Yamoto wapo ndani humu, nimekuja kukata midomo domo, kwa sababu tusiwe tunaongea tu inafika wakati ukweli midomo inaumba, Mkubwa na Wanawe ina watoto 102, kwa hiyo fella anatengeneza vingi, kuna watu wananikwaza, inatakiwa hata siku moja na mimi nipewe certificate ya kusaidia mtaa, kila siku wananibomoa wananibomoa, nisifieni kabla sijafa ninachokifanya hiki”, alisema Mkubwa Fella.

Pia Mkubwa Fella alisema anayajua madai kuwa amewadhulumu Yamoto band, lakini ukweli ni kwamba vijana hao mpaka sasa kila mmoja ana nyumba yake, kitu ambacho kimetokana na juhudi zake

eatv.tv

Comments

comments


Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364