-->

Msami Afuta Kauli Yake, ‘Irene Uwoya Alinitongoza’

Baada ya msanii wa Bongo Flava, Msami kutoa kauli kuwa aliyekuwa mpenzi wake, Irene Uwoya ndiye aliyemtongoza, muimbaji huyo ameamua kuomba radhi kwa kutoa kauli hiyo.

Msamii amesema asingependa kuona mjadala huo unaendelea kwa sasa na anatamani mashabiki wa Irene waendelee kushabikia kazi zake na mashabiki wake pia waendelee kushabiki kazi za Irene, kwani ndio njia ya kuongeza fan base.

“Labda nimeongea vibaya nimemkwaza mtu I say sorry, naomba nisamehewe mimi ni mwanadamu labda naweza nikawa nimeropoka lakini namkubali Irene ni mtu ambaye nimeishi naye vizuri sana ameonyesha moyo mzuri sana, tukiwa pamoja, haitatokea nisema Irene ni mtu mbaya kwangu,” Msamii ameiambia E-Newz ya EATV na kuongeza.

“Sitaki kuiweka hiyo (kauli) tena kwa sababu nitarudi kule tena kwenye kuongea vitu pengine vinaweza kumkwaza mtu, ok naweka sawa… Mimi nilimtokea Irene…  chochote nitakachokuwa nimesema vibaya lets kill it,” amesisitiza.

Msami ambaye kwa sasa anafanya vizuri na ngoma mpya ‘So Fine’ aliyomshirikisha Chemical alikuwa mapenzini na mrembo huyo kutoka Bongo Movie kabla ya kutibuana.

By Peter Akaro

Bongo5

Comments

comments


Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364