-->

Msami Aufungukia ‘Step by Step’

MSANII wa muziki wa kizazi kipya, Msami Giovan ‘Msami’, amesema katika kazi zake zote alizowahi kufanya hadi sasa, wimbo unaomvutia na kumpa hisia kubwa ni ‘Step by Step’.

Akizungumza hivi karibuni jijini Dar es Salaam, Msami alisema wimbo huo umekuwa ukimvutia kila anapousikia, hasa upande wa sauti za vinanda zilizotumiwa.

Alisema kazi hiyo imekuwa ikimburudisha na kumpa faraja ya kuendelea kujituma zaidi ili kuhakikisha anafika mbali katika tasnia nzima ya muziki.

“Step by Step ni wimbo wangu ambao umekuwa ukinipa faraja sana, si kwamba kazi zangu nyingine nilizofanya hazivutii hapana, ila vinanda na zile sauti za vifaa mbalimbali vilivyotumika ndani ya wimbo huo ni sababu,” alisema Msami.

Msami alisema matarajio yake ni kufanya kazi bora zaidi ya zile zilizopita nyuma, huku akiwaomba mashabiki na wadau wa muziki wake kuendelea kuonyesha ushirikiano wa kuzipenda na kutoa ushauri kwenye kazi anazozifanya.

Mtanzania

Comments

comments


Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364