-->

Mahakama yaamuru mke amuache mumewe kwa kutokujenga choo

Mahakama moja katika jimbo la Rajasthan nchini India imemuru mwanamke mmoja kuachana na mumewe wa ndoa, kwa sababu nyumba yao kukosa choo kwa muda mrefu.

Wanawake katika jimbo la Rajasthan nchini India wakienda maporini kwa ajili ya kujisaidia.

Jaji wa Mahakama ya Bhilwara, Rajendra Kumar Sharma, amesema kuwa kwa vile mume hakumjengea choo ndani ya nyumba, katika miaka mitano ya ndoa, basi huo ni ukatili wa kijinsia na hana budi kurudi kwao.

Jaji amesema kwenda kufanya haja maporini ni kitu cha aibu, na ni kumuadhibu mwanamke na kukosa kumuweka salama kwani ni jukumu la mwanaumme.

“Inauma sana tunapowaona mama zetu, dada zetu wakienda maporini kujisaidia nyakati za usiku au alfajili huu ni udhaliulishaji wa kijinsia hauvumiliki Wanaume pesa zao wanatumia kununulia simu, kunywea pombe na kuvutia sigara lakini wamesahau vyoo hili litakuwa fundisho bila shaka”,amesema jaji Kumar kwenye mtandao wa mahakama hiyo wa LawRato.

Shirika la kuhudumia watoto la Umoja wa Mataifa (UNICEF) limesema kuwa karibia watu milioni 600 nusu ya watu wote nchini India hawana vyoo.

Mwaka uliopita 2016, mwanamke mmoja nchini humo alikataa kuolewa katika jimbo la Uttar Pradesh baada ya mwanamume kukataa kujenga choo.

Bongo5

Comments

comments


Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364