-->

Msando Awafungukia Gigy Money na Amber Lulu

Mwanasheria machachari na kipenzi cha wasanii wengi Albert Msando ambaye mara nyingi hujitokeza kuwatetea kwenye masuala ya kisheria, amefunguka kuhusu kuwa karibu na Gigy Money na Amber Lulu, ikiwa mmoja wao alishampa skendo chafu.

Akiongea kwenye kipindi cha Planet Bongo cha East Afrika Radio, Albert Msando amesema anawakubali wasanii hao kwa sababu ni mabinti ambao wanapigana kupambana na maisha.

“Bado nawakubali kama wasanii, nawakubali kama watu ambao wanapambana kwenye maisha, kwa sababu ni wapiganaji, unajua kwenye maisha kuna njia nyingi ambazo ukipambana unaweza kufikia malengo yako, na ni mabinti ambao wanafanya vizuri kwenye kile ambacho wanakifanya”, alisema Albert Msando.

Albert Msando aliwahi kupata na kashfa ya kuwa na mahusiano na msanii Gigy Money ambaye ni maarufu kwa kupiga picha za utupu, kitendo kilichomsababishia kuachia ngazi nafasi yake ya mshauri wa masuala ya kisheria katika chama cha ACT -Wazalendo .

EATV.TV

Comments

comments


Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364