-->

Msanii Bora 2016 Kwangu ni Dogo Janja- Nick II

Rapa Niki wa Pili kutoka katika kundi la Weusi amefunguka na kusema kuwa kwa mtazamo wake kwa mwaka 2016 msanii bora kwake ni Dogo Janjakwani msanii huyo ameweza kufaulu kwa kiwango cha juu mtihani ambao unawashinda wasanii, wasomi, wafanyabiashara wengi duniani.

dogo-janja45

Niki wa Pili anasema Dogo Janja aliwahi kuteleza na kuanguka lakini ameweza kufanikiwa kuinuka katika kiwango cha juu mno huku akiwa na nidhamu ya hali ya juu na kuweza kufuta makosa yake, na sasa anafanya show kubwa ambazo zinaacha historia, lakini amekuwa na ‘Confidence’ iliyovuka mipaka ukilinganisha na umri wake.

“Abduli kachaa A.K.A Dogo Janja kijana mdogo aliyefaulu kwa maksi za juu somo lililowashinda mamilioni ya watu, wasomi, wafanyabiashara, wanamichezo. Watu wa rika zote..somo la kuanguka na kuinuka katika ubora wa kiwango cha juu, nidhamu, kufuta makosa yote..show zake sasa zinaacha history, brand yake iko na professional look, confidence iliyovuka mipaka..kwa umri wake na aliyo ya fanya 2016…namtangaza kuwa msanii wangu bora 2016” Niki wa Pili

 

Comments

comments


Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364