Lord Eyes Amuombea Chid Benzi
Rapa Lord Eyes kutoka katika kundi la Weusi amefunguka na kumtaka msanii Chid Benzi kutopagawa kwani yeye bado ni msanii mkali sana mwenye uwezo wa hali ya juu hivyo anazidi kumuombe kwa Mungu ili aweze kutoka katika mambo ambayo yanamchanganya pia amemkumbusha kuwa anapaswa kumuomba Mungu kwani kila jambo linawezekana.
Lord Eyes alisema hayo kupitia kipindi cha eNEWZ na kusema kuwa Chid Benzi alisikilize sana maneno ya watu bali azidi kumuomba Mungu msaidie kwani kila jambo linawezekana katika dunia hii.
“Pia yeye namuombea Mungu Chid Benzi, Chuma King Kong namwambia nini asipagawe yaani yeye ni MC mkali sana hivyo asipagawe, namwambia asipagawe najua hajapagawa ila asipagawe, siyajui maisha yake kwa sasa lakini ni mwanangu namuombea Mungu kwani sijamuona siku nyingi nina uhakika atakuwa ‘fresh soon as possible’ kwa Mungu kila kitu kinawezekana namkumbusha pia amuombe sana Mungu” alisema Lord Eyes