Msanii Sio Malaika – Irene Uwoya
Malkia wa filamu Bongo, Irene Uwoya amefunguka kwa kusema anachukizwa na tabia za baadhi ya mashabiki waliopo mitandaoni kushindwa kutoa ushauri kistaarabu na badala yake kuanza kuwashambulia kwa kuwatukana.
Uwoya ameeleza hayo baada zile kelele za wasanii wengine kudai mashabiki zao ndiyo wamekuwa vinara katika kuwakosoa pindi wanapokuwa wame-post kazi zao hata muda mwingine maisha yao binafsi wakiwa sehemu wana-enjoy na marafiki zao.
“Mashabiki zetu wapo katika nafasi nzuri ya kusema kama tunakosea au tunapatia lakini njia wanayoitumia kutuelewesha siyo nzuri, wanatumia matusi badala ya kumwambia mtu taratibu akaelewa. Wanasahau kwamba wasanii ni binadamu kama binadamu wengine so tunavyoishi tunaishi kama watu wengine tu. Msanii siyo malaika, saa zingine hawajui mtu unakuwa katika hali gani, labda umefiwa au unaumwa wao wanatukana tu.” alisema Uwoya.
eatv.tv