-->

Msisikilize Maneno ya Watu-Chid Benz (Video)

Rapa Chid Benz ambaye sasa anafanya poa na wimbo wake ‘Muda’ akiwa ameshirikiana na mkongwe Q Chillah amefunguka na kuwataka mashabiki wake kutosikiliza maneno ya watu na kudai wapinzani wake wamekuwa wakimuongelea vibaya kwa lengo la kumchafua.

Chid Benz anasema muda mwingine kwenye maisha yake ya kila siku amekuwa ni mtu wa utani sana kiasi kwamba utani mwingine huwa hapendi hata ufike kwenye ‘Camera’ za watu kwa kudai unaweza kutafsiriwa ndivyo sivyo.

Rapa huyo ameibuka na kusema hayo ikiwa ni siku moja imepita toka alipotoa kauli kwamba anataka kumleta marehemu 2Pac nchini na kusema msanii huyo wa Marekani ni mzima na wala hajafa na kudai tayari wameshafanya naye wimbo.

Comments

comments


Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364