-->

Mahakama Yakataa Vielelezo Kuhusu Kesi ya Wema Sepetu

Mahakama ya hakimu mkaazi Kisutu Jijini Dar es salaam imekataa kupokea vielelezo vya ushahidi wa msokoto na vipisi viwili vya bangi vilivyotolewa na upande wa mashtaka katika kesi inayomkabili Wema na wenzake.

Hakimu Mkazi Mkuu, Thomas Simba alisema Mahakama haiwezi kupokea vielelezo hivyo kwa sababu vina kasoro

“Nakubaliana na hoja kwamba msokoto wa bangi na vipisi vina kasoro kwa kuwa shahidi hakuvifafanua Mahakamani”

Hiyo imekua habari njema kwa Wema Sepetu na wengine walie upande wake ambapo baada ya maamuzi hayo ya Mahakama Wema Sepetu alionekana mwenye furaha na kukumbatiana na wafuasi wake akiwemo Mama yake mzazi.

Alichokisema baada ya kutoka Mahakamani ni hiki “nimefurahi kwasababu naona kabisa kwamba haki inatendeka, nawashukuru Mawakili wangu, tunasubiria hiyo siku September 12″

 

Comments

comments


Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364