Richie Amgeukia Dkt Cheni na Uigizaji
Muigizaji wa filamu bongo, Rich Richie, Single Mtambalike amemtaka muigizaji wa zamani, Dkt. Cheni ambaye kwa sasa amejikita katika ushereheshaji wa shughuli , kurudi kwenye uigizaji kwani kilio chake cha soko la filamu wameshalitatua.
Akizungumza na eNewz ya EATV, Mtambalike amesema kuwa anajua Dkt. Cheni alikata tamaa na kuendelea na kuigiza kwa sababu ya Soko kutokuwa rafiki na waigizaji.
“Nataka nimwambie Dkt. Cheni kwamba ni mzuri kwenye uigizaji na soko linamuhitaji. Kilio alichokua kila siku akilia tumekipatia ufumbuzi. Tumekuja na hii Project ya Barazani na tunawashukuru EATV mnatusapoti naamini tutawafikia watu wengi zaidi kwa mfumo huu kwa hiyo ndugu yangu Cheni usikate tamaa wewe unaweza njoo tuendeleze tasnia,” Mtambalike.
Pamoja na hayo Mtambalike amewaondoa hofu waigizaji wenzake kuhusu Barazani na kuwaambia hawatauza ‘Master’ za movie zao kama jinsi walivyokuwa wanauza hati miliki za filamu na badala yake wao wamekuja kuwakomboa wasanii.