-->

Shamsa ajitosa ishu ya Hamisa na Diamond, ‘hakuna mwanaume asiye-cheat’

Msanii wa filamu Bongo, Shamsa Ford ametia neno kile kinachoendelea kwa sasa kati ya Diamond Platnumz na Mwanamitindo Hamisa Mobetto.

Mapema leo hii Diamond amekiri kuwa mtoto wa Hamissa ni mwanaye licha ya kuwa katika mahusiano na Baby Mama wake, Zari The boss Lady. Katika mtandao wa Instagram Shamsa ameandika ujumbe mfupi na kueleza kuwa Zari anastahili pongezi kwa kujua yote na kuamua kukaa kimya.

Kiukweli anasitahili pongezi kubwa sana, najaribu kuvaa viatu vyake kama mwanamke nayaona maumivu yake la pamoja na yote hakuna mwanaume asiyecheat. Zari endelea kumpenda Nassibu wako kamwe usimuache kwa ajili ya mwanamke mwenzio. NCHI YAKO IKIVAMIWA UNATAKIWA KUPAMBANA NA SI KUKIMBIA.

Ujumbe wa Shamsa ni katika post ya Steve Nyerere ambaye naye aliandika, “Wewe ni Malkia wa nguvu na yote yaliyopita bado umesimama na mmeo kuangalia watoto, Be Strong”.

 

Comments

comments


Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364