-->

Mussa Banzi wa Filamu ya Shumileta na Msiuka Arudi Ramsi Kwenye Filamu

Muongozaji mkongwe wa filamu na mwandishi wa stori za filamu, Mussa Banzi baada ya ukimya wa muda mrefu ameamua kurudi kwenye game la filamu ili kufanya mapinduzi.

musa banzi2

Banzi ambaye aliwahi kutamba na filamu kama Shumileta, Msiuka pamoja na Odama ambayo ilimtoa msanii Odama, ameiambia Bongo5 kuwa ameamua kurudi baada ya kuona tasnia ya filamu inayumba kutokana na kukosa ubunifu.

“Wakati nyingine inabidi ukae kimya ili uangalie soko au tasnia kwa ujumla inaendaje, sio kila wakati uonaonekana wewe tu,” alisema Mussa Banzi. “Lakini nilivyorudi nimekuta malalamiko kidogo, kwamba kiwanda kinaanza kuporomoka kutokana na watu kukosa ubunifu, ndio maana wakongwe tumepigiwa simu na tumekuja ili kuangalia tufanyaje ili kulirudishwa upya soko la filamu,”

Pia Mussa Bandi amesema amekuja na filamu mpya iitwayo Queen Elizabeth.

“Kuna filamu mpya ambayo itatoka mwezi huu, inaitwa Queen Elizabeth. Pia mwaka huu nataka kufanya kitu kipya, kuna filamu ambayo tulifanya miaka ya nyumba na ilivunya rekodi, Odama, hii filamu ndio iliyomtambulisha huyu msanii Odama na mpaka leo yupo safi, lakini mwaka huu tumepanga kuandaa filamu, Gold Odama, yaani Odama wa dhahabu. Kwa hiyo mashabiki wakae mkao wa kula huu ni mwaka wa kazi,” alisema Mussa Banzi.

Bongo5

Comments

comments


Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364