-->

Muziki Umenipa Mafanikio Kuliko Filamu-Shilole

Msanii wa muziki wa bongo fleva Shilole amefunguka na kusema kuwa mafanikio yake aliyopata kwenye muziki kama angeendelea kufanya filamu anaamini asingeweza kuyapata kabisa.

Shilole anasema anashukuru Mungu aliweza kumshtua mapema ili akimbie kwenye filamu na kukimbilia kwenye muziki kwani huku kwenye muziki ndiko pesa zake zilikuwepo ambazo ndani ya muda mfupi amezipata na kufanya mambo makubwa katika maisha yake.

“Namshukuru Mungu nimefikisha miaka 28 najivunia mafanikio yangu katika umri huu nilionao, nashukuru kweli kwani tayari nina bonge la mjengo na miaka yangu 28, nina watoto wawili, na biashara zingine za hapa na pale ikiwepo biashara ya chakula” alizungumza Shilole.

eatv.tv

Comments

comments


Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364