-->

Mwakifwamba Atoa Onyo Kali kwa Wasanii

RAIS wa Shirikisho la Filamu nchini (TAFF), Simon Mwakifwamba, amewaonya wasanii wa filamu na wale wanaounga mkono Shirikisho hilo kutogombana na amewataka waungane kwa ajili ya kufanya kazi.

MWAKIFWAMBA

Simon Mwakifwamba

Akizungumza na MTANZANIA, Mwakifwamba alisema kuwa kwa muda mrefu kumekuwa na hali ya vuta nikuvute baina ya makundi hayo ya wasanii ugomvi uliochangia kuirudisha nyuma tasnia hiyo

“Tunashukuru ugomvi umeisha, sioni sababu ya wasanii kurudia hiyo tabia ya kutupiana vijembe kwani hatujengi bali tunabomoa hivyo basi adhabu kali itatolewa kwa yeyote atakayeibua ugomvi tena,” alisema Mwakifwamba.

Aliongeza mara baada ya ugomvi huo kumalizika, TAFF wana mpango wa kuunda umoja wa wasanii wote ili uwasaidie kufanya kazi zitakazoifikisha mbali tasnia hiyo.

Comments

comments

Post Tagged with

Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364