-->

Mwakyembe:Bifu la Diamond na Ali Kiba wacha liendelee

Waziri wa habari utamaduni na michezo DKT. Harrison Mwakyembe amesema bifu la Diamond na Ali Kiba linafaa kuendelea sababu linaleta tija kwenye muziki.

“Kama kuna ushindani kati ya Alikiba na Diamond ambao ni kiuweledi, kitaaluma basi mimi nafikirii tungeuendeleza zaidi, hamna sababu ya kuwasuluhisha, waendelee kushindani vizuri tupate muziki bora.”

“Kwa hiyo mimi naomba Watanzania wachukulie mvutano huo ni mzuri katika tasnia, mradi mimi sijasikia watu wameshikiana mapanga,” ameongeza.

Katika hatua nyingine Dkt. Mwakyembe ameendelea kusisitiza dhamira yake ya kuwaita pamoja Diamond na Alikiba ili kufanya ngoma pamoja kama alivyowahi kuhaidi hapo awali.

“Ukifika muda nitawaita wote watanisikiliza tu watatunga wimbo mmoja wa kukata na shoka pengine bara nzima la Afrika litatikisika, ni vijana wenye vipaji lazima tuendelee kuwatia moyo,” alisema Waziri.

Mwanaspoti

Comments

comments


Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364