Mwanaume Mfupi Kwangu Hapana – Shilole
Msanii Shilole amefunguka na kuweka wazi kigezo kimoja wapo anachoangalia katika kumkubali mtu au kumtokea kuwa kuwa naye katika mahusiano na kusema kimo cha mtu kwake ni kigezo moja wapo.
Shilole alisema hayo alipokuwa kwenye kipindi cha KIKAANGONI kinachofanyika kupitia ukurasa wa facebook wa EATV, wiki mbili zilizopita na kudai saizi yeye kutoka kimapenzi na mtu mfupi ni jambo gumu kwani anavutiwa zaidi na watu warefu wenye kimo cha kutosha na si wanaume wafupi.
“Mimi napenda mwanaume yoyote yule ilimradi anajitambua basi, suala la muonekano hilo linatengenezwa ila kiukweli kabisa mimi napenda mwanaume mrefu, mwanaume mfupi kwangu hapana, Barnaba yeye ni mfupi na kila mmoja ameumbwa na Mungu tofauti, ila sasa hivi vigezo na masharti kuzingatiwa” alisema Shilole
Mbali na hilo Shilole anasema anapenda sana kuolewa ili na yeye awe na heshima yake kama mke
“Napenda kuolewa na mimi niwe na heshima yangu, niwe na mume wangu basi hamna mtu asiyependa kuolewa, ndoa ni heshima ndiyo maana unasikia watu wanasema mke wa fulani yule, muwe wa fulani yule lakini siyo aah yule si mwanamke tu kwa hiyo ndoa ni heshima” alisisitiza Shilole
eatv.tv