-->

Mwanaume Wangu wa Sasa sio Serengeti Boy-Shilole

Msanii wa muziki wa kizazi kipya asiyeisha vituko Shilole amemtetea mwanaume wake mpya baada ya tuhuma za kutoka na serengeti boys.

Akizungumza kwenye kipindi cha Planet Bongo cha East Africa Radio, Shilole amesema kwa sasa yeye hana mahusiano na wanaume ambao amewazidi umri, kwani mpenzi wake wa sasa ni mwanaume halisi (gentle man) na amemfanya awe na mawazo ya kuwa mke.

“Mwanaume wangu wa sasa sio serengeti boys, ni gentle man, anajielewa na pia ni mtu mzima, ananifanya mpaka nifikirie kuolewa niwe mke, yaani sio serengeti boy kabisa, na pia hataki kabisa mambo ya mitandao na ndio maana simuweki wazi”, alisema Shilole.

Hata hivyo Shilole ambaye leo ameachia wimbo wake mpya unaoitwa ‘Kigori’, amewatetea watu ambao wana mahusiano na wanaume wanaowazidi umri (serengeti boys) na kusema siyo kitu cha ajabu kwani umri ni namba tu, kinachomata ni mapenzi.

“Kwani kitu gani…!! age is just a number, watu wanaangalia mapenzi bwana so its not a big deal kuwa na kiserengeti”, alisema Shilole.

Hapo nyuma Shilole alishawahi kukumbwa na sakata la kuwa na mahusiano na wanaume wenye umri mdogo (serengeti boys) akiwemo aliyekuwa mpenzi wake Nuhu Mziwanda.

EATV.TV

 

Comments

comments


Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364