-->

Mau Fundi na Filamu ya Mwalimu Masemele

FILAMU ya Mwalimu Masemele iliyotayarishwa na muigizaji nyota Maulid Ally aka Maufundi imeingia sokoni leo na inasambazwa nchi nzima kwa maduka yote ambayo yanauza filamu za kibongo sinema hiyo imeandaliwa mkoani Morogoro lengo la mtayarishaji ikiwa ni kuwaweka pamoja wasanii wote.

Akiongea na FC Mau amesema kuwa filamu hiyo ni nzuri na ina mafunzo kwa jamii huku ikiacha burudani kwa mtazamaji ambaye ana haki kuipata kwani kuna waigizaji mahiri katika filamu hiyo ambao kama walikuwa katika mashindano, Mau anasema wameitendea haki filamu hiyo.

Maufundi mwigizaji wa filamu

“Muziki huu si wa kitoto maana unakutana na King mwenyewe yaani King Majuto na Prince wake mwenye Mau fundi kuna nini hapo! Lazima watunyooke, filamu hii inasambazwa na Auguster Company ltd,”alisema alisema.

Sinema hiyo imeongozwa na muongozaji Henry Mwakajumba ikishirikisha wasanii kama vile King Majuto, MauFundi, Monica Sizya, Ramia Lulandala, Muki Abdalah, mpiga picha ni Said Dizele na wasanii wengi kibao.

Mau fundi akiwa location kurekodi filamu ya Mwalimu Masemele.

Filamucentral

Comments

comments


Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364