-->

Mzee Jangala Awaingiza ‘Jandoni’ Wasanii Vijana

Mkongwe wa sanaa za maigizo nchini Mzee Jangala amewachana wasanii wa kiume wanaovaa nguo zinazobana, kutoboa masikio na kuonesha maumbile yao.

Akiongea kupitia eNewz amesema vijana wanapaswa kujitambua na kuelewa maana ya utandawazi na siyo kuiga mambo mbalimbali ikiwemo kukaa uchi mbele za watu wazima kubadilisha maumbile yao halisi na kudai kuwa wanafuata utandawazi na kupotosha jamii zima.

Hata hivyo Mzee Jangala hakusita kuwasihi wasanii wa kizazi kipya kujitambua na kufanya mambo ya msingi katika jamii kwa kuwa wao ni watu ambao wana mashabiki ambao wanawaufatilia maisha yao na kuiga kila kinachofanywa na watu maarufu.

Mtazame Jangala katika video hii ya kipindi cha eNewz

Comments

comments


Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364