-->

Mzee Majuto Aanika Mafanikio Aliyoyapata kwenye Sanaa

Msanii wa vichekesho Mzee Majuto amefunguka na kusema sanaa imembadilisha maisha na kudai ameweza kujenga nyumba kubwa tatu, ameweza kununua magari matano pamoja na kumiliki shamba lenye ukubwa wa ekari tano.

Mzee Majuto amedai kuwa ameanza kufanikiwa katika sanaa baada ua kuanza kujitegemea mwenyewe kwenye kazi zake, hivyo amedai kwa mafanikio ambayo amepata sasa inatosha
ameamua kuachana na kazi hiyo ya kuingiza, ingawa anasema matangazo yupo tayari kufanya ila si uigizaji tena.

“Zamani sanaa ilikuwa ya mkandamizano sana lakini baadaye nilipata mafanikio nilikuwa sina nyumba saizi nina nyumba tatu, nikaweza kuwa na magari matano hiace nne na Noah moja na nikaweza kusomesha watoto wangu wengine wakifika mpaka chuo kikuu, nashukuru Mungu nimejenga msikiti na madrasa nina shamba langu kubwa zuri tu, hivyo nasubiri safari ambayo haina kipingamizi lazima tuondoke ambayo ni kufa, kwa hiyo saizi mimi sanaa basi labda mtu akiniita kuna tangazo nitamfanyia tangazo lake nikimaliza narudi shambani kwangu kumtumikia Mungu na kuomba toba” alisema Mzee Majuto.

Wiki kadhaa zilizopita Mzee Majuto alifanyia upasuaji kutokana na tatizo lake la ngiri lakini mpaka sasa anaendelea vyema , hata hivyo leo Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo Dr. Harrison Mwakyembe alimtembelea Mzee Majuto nyumbani kwake jijini Tanga na kumpa pole kwa kuugua.

Comments

comments


Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364