-->

Mzee wa Upako Awafungukia Bongo Movie

Mchungaji wa Kanisa la Maombezi (GRC), Anthony Lusekelo alimaarufu kama ‘Mzee wa Upako’ anashangaa Waigizaji wa Bongo Movie kwa kuigiza vitu ambavyo havina uhalisia kama filamu za wenzetu walioendelea.

Mzee wa Upako amesema anawashangaa Waigizaji hao kuandamana kwa kudai wanaharibiwa soko na filamu za kigeni ile hali vitu wanavyoigiza havina uhalisia kabisa kwenye jamii yetu kwani utakuta mtu anaigiza kama Meneja wa kampuni kubwa lakini utakuta kavaa hereni na nywele kaweka dawa.

Vijana wa Bongo Movie wanalalamika kuwa hawana soko lakini soko wameharibu wenyewe… utakuta mtu katika sinema moja anaanza kuwa shemeji wa mtu fulani inaisha anakuwa kaka sasa hawa jamaa mimi….mhhhhh !!”amesema Mzee wa Upako huku akiendelea kuhoji kwa mshangao

Unajua uhalisia ni jambo muhimu sana yale ambayo hatuyawezi ndiyo tunaingiza mimi huwa nawashangaa sana!!… hivi ndugu yangu unawatengenezea sinema Watanzania una act kama Meneja wa TRA halafu umevaa heleni na nywele umeweka kalikiti hivi kuna Meneja gani hapa Tanzania anavaa heleni?, Uhalisia ule lazima uwepo ule ambao hatuuwezi ndiyo huwa tunaigiza lakini wewe unasema Meneja wa TRA, Boss kabisa unawafanyakazi halafu umeweka nywele dawa na umevaa heleni!!,“amesema Mzee wa Upako kwenye mahojiano yake na Chomoza ya Clouds Tv.

Hata hivyo Mchungaji Lusekelo hakuishia Bongo Movie tuu amewashauri pia Wasanii wa muziki wa injili kuwa wamoja kama walivyo Wasanii wa Bongo Fleva kwa kufanya kolabo nyingi.

Bongo5

Comments

comments


Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364