-->

Namchukia Mwanaume Aliyenipa Mimba – Nisha Bebe

Msanii wa bongo movie Nisha Bebe amesema ujauzito wake unampa hisia tofauti na mawazo mpaka anafikia hatua ya kupost mambo tofauti tofauti kwenye mitandao yake kwa kuwa hampendi mwanaume aliyempa ujauzito huo.

nisha33

Akiongea ndani ya eNewz Nisha amesema amevumilia miezi mitano bila mtu kujua kitu chochote juu ya mimba yake lakini kwa sasa ameshindwa kuvumilia na hiyo ni kutokana na maumivu anayoyapata na kwamba mimba aliyoibeba ni ya mtu ambaye hampendi tena.

Pia Nisha amesema mwanaume aliyempa mimba ni mtu ambaye anapenda kujionesha sababu ambayo ilipelekea wakaachana pia Nisha amesema anamuomba Mungu mtoto wake asifanane na baba yake na kama ikitokea akifanana naye hatakuwa budi ya kumficha bali atampa mtoto wake kila anachokitaka kwa kuwa mtoto hana kosa lolote.

nisha943

eatv.tv

Comments

comments


Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364