-->

Namiliki Fremu Zaidi ya 70 – Z Anto

Msanii wa muziki wa kizazi ambaye aliwahi kutamba na ngoma kama Binti kiziwi, Mpenzi jini na Kisiwa cha Malavidavi Z Anto amefunguka na kusema kuwa hapa mjini anamiliki fremu za biashara zaidi ya 70.

Z Anto anasema kuwa yeye ni kama baadhi ya wasanii ambao wamekuwa na maneno mengi kuliko utekelezaji ndiyo maana amekuwa akizidi kufanikiwa katika mambo yake licha ya kuwa kimya kwenye muziki kwa muda mrefu.

Z Anto anakiri kuwa sasa anataka kurudi rasmi kwenye muziki ila hafanyi muziki ili kuendesha maisha yake bali anataka kufanya muziki kama njia ya kupanua biashara zake na kusema mpaka sasa kazi yake mpya imeshakamilika hivyo muda wowote anaichia.

“Mara nyingi wasanii huwa wanakuwa na maneno mengi pasipo vitendo lakini kama tungekuwa karibu na mazingira yangu ya biashara ningekwambia angalia aina ya biashara ambayo naifanya labda ungepata jibu nafanya biashara ya aina gani lakini mimi ni mmiliki wa fremu za biashara zisizopungua sabini na kitu hivi, lakini pamoja na hivyo nina biashara zingine kama za magari, hata uongozi wangu mpya ambao mimi nimeutengeneza utakuwa unadili na biashara kama hizo na kubwa kuliko hizo tena lengo letu si kuingia kwenye sanaa kutegemea show na dili za sanaa kama zilivyo hapana tunataka kuingia kwenye sanaa tufanye kama wasanii wa nje wanavyofanya,” alisema Z Anto

Z Anto aliendelea kusisitiza kuwa muziki ambao anataka kufanya sasa ni kama mtaji na kufungua njia za biashara zake zingine zaidi lakini si kufanya muziki kwa ajili ya kutegemea show tu peke yake, yaani anataka kutumia muziki kufungua milango mingine ya biashara.

“Wasanii wenzetu wa mbele wanakuwa na kampuni sijui za maji, na vitu vingine wakati wakiendelea na sanaa yao kwa hiyo hata mimi nataka kuingia kwenye biashara nyingi tofauti tofauti kwa hiyo sanaa ni kama mtaji kwangu lakini tofauti na hapo na biashara zingine za magari pia nina biashara zingine za kifamilia nilikuwa nasimamia ndiyo zilikuwa zikinifanya kuwa busy kwa muda mrefu kwa hiyo maisha yanakwenda kwa namna hiyo” alisema Z Anto

Mbali na hilo Z Anto anasema maandalizi ya kazi yake mpya yamekalimika kwa asilimia 98 kwani tayari ameshaunda menejimenti, ameshakamilisha video ipo tayari na kusema kila kitu kipo sawa kilichobaki ni kusema tu siku ya kazi hiyo ambayo inatakiwa kutoka.

EATV.TV

Comments

comments


Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364