Afande Sele Atoa Ujumbe Huu kwa Kina Baba Wote
Ikiwa leo ni siku ya akina Baba Duniani Mfalme wa Rhymes nchini Tanzania, Afande Sele amewaasa akina Baba wote ulimwenguni kukumbuka majukumu yao kwa watoto na sio kuishia kuwapa mimba tuu akina mama bila kutunza watoto.
Afande Sele ambae ni mtoto Baba wa watoto wawili amesema jukumu la Baba lisiishie kutia mimba tuu bali lije mpaka kwenye matunzo ya mtoto.
“Leo Ni Siku Yetu Akina Baba…Jukumu Letu Lisiishie Kutia Mimba tu Nakuitwa Baba Mwenye Nyumba…Tumeagizwa Upendo…Tena Kwa Vitendo…“ameandika Afande Sele kwenye ukurasa wake wa Instagram.
Bongo5