-->

Snura Adai Kusumbuliwa Sana na Wanaume Hawa

Msanii wa muziki Snura Mushi alimaarufu kama Snura Majanga amefunguka na kusema kuwa amekuwa akipata shida sana na wanaume mbalimbali wenye matamanio kutokana na vile anavyoweza kutumia mwili wake kwenye uchezaji wake akiwa stejini.

snura567

Snura alizungumza haya kwenye kipindi cha Planet Bongo ya East Africa Radio na kusema kuwa licha ya kupata usumbufu huo kwa wanaume hao lakini amekuwa akijitunza na kujiheshimu kwani anafanya hivyo kulinda kazi yake na heshima yake kama mwanamke.

“Unajua watu wakisikia Snura Chura huwa wanatokea wengi sana, na kweli huwa napata shida sana kwa wanaume wengi wenye matamanio, na inawezekana kweli kati yao wapo wenye mapenzi ya kweli na mimi lakini ndiyo hivyo, kitu nachozingatia sana ni kuilinda kazi yangu, hivyo wanapotokea wanaume wa namna hii mimi nachokifanya siku zote ni kuwa mbali nao kabisa ndiyo maana nashinda vishawishi hivyo kila siku” alisema Snura

eatv.tv

Comments

comments


Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364