-->

Wastara Amnasa Kigogo Morogoro

IMEVUJA! Safari za mara kwa mara mkoani Morogoro, zinazofanywa na staa wa filamu za Kibongo, Wastara Juma zinadaiwa kuchangizwa baada ya kumnasa kigogo mmoja mkoani humo.

Wastara341

Chanzo makini kililiambia Risasi Mchanganyiko kuwa muigizaji huyo amempata mfanyabiashara na kiongozi wa serikali mkoani humo, kitu kinachomfanya afanye safari zaidi ya mara nne kwa mwezi.

“Yaani siku hizi Wastara hatulii Dar ilipo familia yake, amekuwa akisafiri Morogoro kila kukicha, yaani hivi sasa ni mapenzi motomoto, lakini ni kwa siri sana hataki ijulikane,” kilisema chanzo chetu hicho.

Baada ya kuunyaka ‘ubuyu’ huo, paparazi wetu alimtafuta Wastara na alipopatikana, alikana taarifa hizo na kudai safari zake za mara kwa  mara mkoani humo ni kwa vile huko ni nyumbani kwao.

“Hizo habari siyo kweli, watu wanapenda tu kuongea, Morogoro huwa naenda kwa sababu ya mambo mawili, kwanza kule ndiko nilikozaliwa hivyo huwa naenda kuwaona ndugu zangu na pili huwa naenda kwa sababu nina kituo cha kulelea watoto yatima, kwa hiyo huwa naenda kuwaangalia,” alisema Wastara.

Chanzo:GPL

Comments

comments


Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364