-->

Nawal Afuta Tattoo ya Nuh Mziwanda!

Ni utamaduni wa mastaa wa Bongo, mara tu wanapoanzisha uhusiano na kukolea kwenye penzi jipya, kujichora tattoo ya jina la mpenzi huyo lakini dhoruba inapolipitia penzi lao, hutafuta kila njia za kufuta tattoo hiyo.

Hili limejidhihirisha kwa aliyekuwa mke wa mwanamuziki wa Bongo Fleva, Nuh Mziwanda, anayefahamika kwa jina la Nawal, ambaye kwa sasa amefuta tattoo ya mzazi mwenziye huyo, baada ya kupigana kibuti na mwanadada huyo kuolewa na mwanaume mwingine anayeitwa Masoud.

Ubuyu wa Nawal kufuta tattoo ya Nuh aliyokuwa ameichora mkononi mwake, umeanza kumung’unywa baada ya kuzagaa kwa picha inayomuonyesha akiwa ufukweni huku mkono wake uliokuwa umechorwa jina la ‘Nuh Mziwanda’ ukionekana kufutwa tattoo hiyo na kuchorwa ua.

Nawal alimkuta Nuh akiwa katika kipindi kigumu huku kichwa chake kikiwa na msongo wa mawazo, zilizotokana na kumwagana na Queen wa Bongo Fleva, Shilole, ambapo alikuja kwa kasi ya 4G na kumtuliza mawazo Mbongo Fleva huyo, akaamua kuchora na tattoo ya jina lake ili kumdhihirishia kuwa anampenda sana.

Penzi lao lilijizolea mashabiki wengi kutokana na jinsi walivyokuwa wamegandana kama ruba, mpaka walipofikia hatua ya kufunga pingu za maisha, wakabarikiwa na mtoto wa kike anayeitwa Anyaghile, kisha ‘Jini Kivuruge’ akaliandama penzi lao na kufanikiwa kuwasambaratisha.

NA ISRI MOHAMED/GPL

Comments

comments


Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364