-->

Mama ni Kila Kitu Kwangu- Riyama

MUIGIZAJI wa filamu wa kike Bongo Riyama Ali anasema kuwa mama yake ni ndio kila kitu katika maisha yake na hata mwanaye anamulelea kwa kumfundisha kuheshimu wazazi, huku akijaribu kumpa miongozo bora kama mzazi anayependa familia yenye malezi bora kwa watoto na jamii nzima kwa ujumla wake.

“Wapo baadhi ya wanadamu ambao hutamani wafanane na wao labda kama wamekuwa watu maarufu au kuwa wanaosifiwa kama wazuri lakini kwangu Mama ni kila kitu hata kama angekuwa kichaa ningempenda tu,”alisema Riyama.

Riyama anasema kuwa mama anapitia changamoto nyingi kuliko hata baba kama mwanamke angekuwa na roho ya kukata tamaa basi jamii ingekuwa imejaa watoto waishi katika mazingira magumu hivyo haina maana kama mama yako ana muonekano mbaya ndio asiwe mzazi wako hizo anaona ni tabia za kitumwa.

Comments

comments


Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364