-->

Nay wa Mitego Afungukia Ishu Yake na Nini

Msanii wa muziki wa kizazi kipya Emmanuel Elibariki maarufu kama Nay wa Mitego, amesema jambo lolote linaweza kutokea kati yake na msanii Nini, ingawa kwa sasa hawana mahusiano.

 

Akizungumza na EATV Nay amesema kitu kilichopo kati yake na Nini kwa sasa ni kazi tu, lakini haitakuwa kitu cha ajabu iwao lolote likitokea baina yao.

“Mimi na Nini ni washkaji tunafanya kazi tu, huenda yeye ana mtu wake, nami nina mtu wangu, hakuna mahusiano yoyote, lakini huwezi jua lolote linaweza tokea, kwani hakuna ubaya”, amesema Nay wa Mitego.

Hapo awali kulikuwa na tetesi kuwa wawili hao ni wapenzi na ndio chanzo cha Nini kuondoka kwenye uongozi wake wa awali, lakini sasa hivi wamekuwa wamekanusha mahusiano hayo.

 

Comments

comments


Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364